- Mwombaji awe na ujuzi wa ufundi ambao aliupata bila kupitia chuo au mfumo rasmi wa mafunzo. Hivyo hana cheti kinachoelezea kuhusu ujuzi alionao.
- Mwombaji awe na uzoefu usiopungua miaka mitano (5) kwenye fani yake.
- Mwombaji awe Mtanzania mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.
- Ujuzi anaoomba kurasimisha uwe miongoni mwa fani ambazo VETA inazirasimisha kwa wakati huo. Fani hizo zimeainishwa katika kipengele kinachofuata.









