Vifurushi vya Bima ya Afya
Vifurushi vya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) vya Tarangire Afya, Ngorongoro Afya, Mikumi Afya, Serengeti Afya na Tanzanite ni mpango unaowezesha mwananchi mmoja mmoja au familia kuchagua na kuchangia huduma za matibabu.
Faida za kujiunga na Vifurushi vya Bima ya Afya
i. Wigo mpana wa huduma za matibabu ya msingi, kibingwa na bingwa bobezi.
ii. Punguzo la asimilia 10 ya mchango wa mtegemezi kwa wanaojiunga kifamilia.
iii. Matibabu nchi nzima katika vituo vya matibabu zaidi ya 10,000 kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Hospitali ya Taifa kwa kuzingatia utaratibu wa rufaa kwa kifurushi cha Ngorongoro, Mikumi, Serengeti na Tanzanite Afya.
iv. Kwa kifurushi cha Tarangire matibabu nchi nzima kuanzia Zahanati hadi hospitali ya rufaa ya Mkoa.






