Home HESLB Documents Za Kuandaa Ili Kuomba Mkopo HESLB

Documents Za Kuandaa Ili Kuomba Mkopo HESLB

6
0

Utahitaji kuandaa taarifa zako binafsi, vyeti vya elimu, nyaraka zinazothibitisha uhitaji (kama yatima au ulemavu), na taarifa za wadhamini. Nyaraka hizi zote zitahitajika kupakiwa kidijitali kupitia Mfumo wa OLAMS HESLB wakati wa mchakato wa maombi.

Sifa za Kuomba Mkopo wa Elimu HESLB

Ili mwanafunzi aweze kuomba na kupata mkopo wa elimu, anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:

  1. Awe raia wa Tanzania.
  2. Awe amepata udahili katika chuo kinachotambulika na mamlaka husika.
  3. Asiwe na uwezo wa kugharamia masomo kwa kujitegemea.
  4. Awe na nyaraka kamili na halali kama vile cheti cha kuzaliwa, vyeti vya elimu, na kitambulisho cha taifa.
  5. Awe hajawahi kunufaika na mkopo wa aina hiyo hapo awali kwa kiwango cha shahada anachoomba.

Ni documents/nyaraka gani muhimu zinatakiwa wakati wa kuomba mkopo?

  1. Cheti cha kuzaliwa cha mwombaji kilichothibitishwa na RITA/ZCSRA
  2. Cheti cha kifo ikiwa umepoteza mzazi kilichothibitishwa na RITA/ZCSRA
  3. Kitambulisho cha mdhamini (NIDA, Mpiga Kura, Leseni ya Udereva au Pasi ya Kusafiria)
  4. Fomu ya ufadhili iliyojazwa kwa usahihi ikiwa ulifadhiliwa katika masomo ya sekondari
  5. Barua ya Mganga Mkuu wa Wilaya au Mkoa ikiwa mwombaji au mzazi wake ana ulemavu
  6. Picha (passport size) za mwombaji wa mkopo na mdhamini wake

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here