Home HESLB Majina ya waliopata Mkopo 2025-2026 – HESLB Loan Beneficiary

Majina ya waliopata Mkopo 2025-2026 – HESLB Loan Beneficiary

747
0

Orodha ya majina wa form six waliopata Mkopo pdf Bodi ya Mkopo HESLB mwaka huu 2025-2026 awamu ya kwanza

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) iko mchakato wa kutangaza majina ya wanafunzi wa Form six ambao ndio waombaji ambao wamethibitishwa kupata mikopo kwa waliohitimu kwa ajili ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2025‑2026.

Majina hayo yatapatikana kupitia orodha rasmi ambayo HESLB itachapisha kwa umma, na wanafunzi wanashauriwa kufuatilia akaunti zao za SIPA au mfumo wa OLAMS ili kujua ikiwa wamejumuishwa kwenye wa walionufaika.

Wakati huu, HESLB inaendelea na ukaguzi na maandalizi ya orodha hizo, ikiwa ni pamoja na uhakiki wa sifa za waombaji na ulinganishaji wa taarifa zao na vigezo vilivyowekwa.

Hivyo wanafunzi wanaotarajia wanashauriwa kuwa wa makini na taarifa kutoka HESLB na kuangalia mara kwa mara ili wasikose kupokea taarifa wakati majina yatakapochapishwa.

 

TAARIFA KWA UMMA

426.5 BILIONI ZATOLEWA KWA WANAFUNZI 135,240

 

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo Ijumaa, Oktoba 24,2025 imetoa awamu ya kwanza ya upangaji mikopo na ruzuku yenye jumla ya wanafunzi 135,240. Idadi hii inajumuisha wanafunzi wafuatato:

 

i. Wanafunzi 40,952 wa shahada ya awali na wanafunzi 5,342 wa stashahada waliopangiwa mikopo kiasi cha TZS. 152 bilioni.

 

ii. Wanafunzi 615 wa Samia Skolashipu waliopangiwa ruzuku kiasi cha TZS. 3.3 bilioni.

 

iii. Wanafunzi 88,331 wanaoendelea na masomo wamepangiwa mkopo kiasi cha TZS. 271.2 bilioni baada ya kufaulu mitihani yao ya mwaka uliotangulia.

 

Bodi ya Mikopo itaendelea kutoa awamu zingine za mikopo na skolashipu kadiri itakavyopokea uthibitisho wa udahili kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza na matokeo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo.

 

Aidha, Bodi ya Mikopo inawakumbusha waombaji wa mikopo na ruzuku kuendelea kufuatilia taarifa za maombi yao kupitia ‘SIPA’ wakati taratibu za uchambuzi na upangaji wa mikopo na ruzuku zikiendelea.

 

 

 

Imetolewa na:

 

Mkurugenzi Mtendaji

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)

Ijumaa, Oktoba 24, 2025

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here