AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA II (AGRICULTURAL FIELD OFFICERS) –
Nafasi 292
MAJUKUMU YA KAZI
• Kushirikiana na watafiti kuendesha vishamba vya majaribio.
• Kukusanya/kuhifadhi takwimu za majaribio,
• Kuwafundisha wakulima mbinu za kilimo bora,
• Kuwafikishia wakulima matokeo ya utafiti,
• Kuwafundisha wakulima mbinu bora za kilimo, matumizi ya mbolea na madawa,
pembejeo za kilimo,
• Kukusanya na kutunza takwimu za mazao na bei kwa wiki mwezi, robo na mwaka
ngazi ya halmashauri,
• Kukusanya takwimu za mvua,
• Kushiriki katika savei za kilimo,
• Kushirikiana na vikundi vya wakulima kuhusu matatizo na teknolojia sahihi za kutumia,
• Kupanga mipango ya uzalishaji,
• Kupima uotaji wa mbegu na kusimamia taratibu za ukaguzi,
• Kutathmini na kusavei maeneo ya vyanzo vya maji kwa ajili ya kuhifadhi,
• Kutunza miti mizazi,
• Kuwatambua wasambazaji wa pembejeo,
• Kutoa mafunzo ya lishe kwa wakulima,
• Kufanya vipimo vya ubora, unyevunyevu na uotaji wa mbegu,
• Kusimamia taratibu za ukaguzi,
• Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea,
• Kusimamia shughuli za kila siku za majaribio ya kilimo,
• Kuwaelimisha wakulima juu ya matumizi bora ya udongo na maji,
• Kutoa ushauri wa kilimo mseto,
• Kuandaa sheria ndogo za hifadhi ya mazingira na
• Kutoa taaluma ya uzalishaji wa mboga, matunda, maua na viungo.
SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha nne au Sita (VI) wenye stashahada (Diploma) ya
kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA
TGS.C
CLICK HERE TO APPLY










