Home AJIRA PORTAL Mwalimu Daraja III C – Fizikia kutoka MDAs & LGAs, 2026

Mwalimu Daraja III C – Fizikia kutoka MDAs & LGAs, 2026

163
0
📢 JIUNGE NA CHANNEL YETU

Nafasi 201 mpya za Ajira na Kazi za Ulimu wa Physics (Fizikia) kutoka Utumishi kupitia MDAs & LGAs kwa mwaka 2026, wenye vigezo wote wanahimizwa kutuma maombiharaka iwezekanavyo.

Kazi na Majukumu

  1. Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa;
  2. Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia;
  3. Kufundisha, kufanya Tathmini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya Wanafunzi;
  4. Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
  5. Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi;
  6. Kutoa ushauri wa Kitaalamu na kutaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;
  7. Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za Shule;
  8. Kazi nyingine atakazopangwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule

Elimu na Vigezo

Kuajiriwa mwenye Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Fizikia au Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Fizikia  pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu  ya Juu vinavyotambulika na Serikali.

BONYEZA HAPA KUTUMA MAOMBI

📢 JIUNGE NA CHANNEL YETU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here