Mtakumbuka kwamba kati ya Mwezi Februari na Juni, 2025 Mamlaka ya Mapato Tanzania iliendesha zoezi la usaili ili kujaza nafasi 1,596 zilizokuwa wazi. Baada ya mchakato ule, waomba kazi waliofikia na kufaulu vizuri zaidi katika hatua ya
usaili wa mahojiano waliajiriwa kujaza nafasi hizo katika kada mbalimbali. Aidha, waomba kazi wengine walifikia na kufaulu usaili wa mahojiano lakini hawakuweza kuajiriwa kutokana na uchache wa nafasi, Mamlaka iliwajulisha kuwa
wamewekwa kwenye kanzidata (Database) na pale nafasi zitakapopatikana wataajiriwa kwa kuzingatia ufaulu wao.
Kwa kuzingatia maelezo haya, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuutaarifu umma kuwa inazo nafasi chache zilizotokana na watumishi kukoma utumishi wao ndani ya Mamlaka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kustaafu kazi kwa mujibu wa sheria ambazo zitajazwa kwa kutumia kanzidata iliyopo.
Hivyo, wanaostahili wanashauriwa kufuatilia barua pepe zao na taarifa rasmi zitakazotolewa na Mamlaka kupitia tovuti yake na kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.









