Ajira Portal ni jukwaa la mtandaoni lililoundwa na sekretarieti ya ajira Tanzania ili kuwawezesha wanaotafuta kazi kutuma maombi ya nafasi wazi katika taasisi na mashirika mbalimbali ya serikali.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Usaili Ajira Portal
Waombaji wanaweza kuangalia matokeo yao kwa kufuata hatua hizi:
Hatua ya 1: Tembelea Ajira Portal
Nenda kwenye mfumo rasmi wa Ajira Portal
Hatua ya 2: Ingia Kwenye Akaunti Yako
Tumia:
- Barua pepe uliyosajili
- Nenosiri lako
Hatua ya 3: Fungua Sehemu ya Matokeo
Baada ya kuingia kwenye akaunti:
- Chagua My Applications
- Fungua Interview Results au Matokeo ya Usaili
Hatua ya 4: Angalia Matokeo
Kama matokeo yameshatolewa utaweza:
- Kuona hali ya maombi yako
- Kupakua PDF ya matokeo
- Kuangalia kama umeitwa hatua inayofuata au umechaguliwa kazini
Links Mhimu
- Matangazo ya Kazi
Link: https://portal.ajira.go.tz/vacancies
Hii ni sehemu yenye matangazo ya kazi, ambapo waombaji wanaweza kuona kazi zote zilizotangazwa kwenye Ajira Portal. - Kuingia kwenye Akaunti
Link: https://portal.ajira.go.tz/auth/login
Hii ni link ya kuingia kwa watumiaji waliosajiliwa tayari. - Maoni na Mrejesho
Link: https://portal.ajira.go.tz/feedback
Hii ni sehemu ya kutoa maoni na mrejesho kuhusu uzoefu na huduma zinazotolewa kwenye Ajira Portal. - Kujisajili kwa Akaunti Mpya
Link: https://portal.ajira.go.tz/auth/register
Hii ni kwa waombaji wapya wanaotaka kujiandikisha kwenye Ajira Portal.











