Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeundwa kwa mujibu wa Ibara ya
62 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977. Aidha,
Ibara ya 88 (1) ya Katiba inaunda Sekretarieti ya Bunge yenye jukumu la
kuliwezesha Bunge kutekeleza majukumu yake.
Kwa msingi huo, Katibu wa Bunge anatangaza nafasi za kazi 28 za Kada mbalimbali
ili kuimarisha utendaji. Watanzania wote wenye sifa na uwezo wanaalikwa kutuma
maombi yao ili kujaza nafasi za kazi kama zilivyoanishwa hapa chini:-
MASHARTI YA JUMLA
1. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45
isipokuwa kwa wale walioajiriwa Serikalini.
2. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa
kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa.
3. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili.
4. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi
kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
5. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo binafsi, nakala za vyeti
vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato
cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika kama vile:
(a) Postgraduate/Degree/Advanced Diploma
(b) Diploma/Certificates.
(c) Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI.
(d) Computer Certificate.
(e) Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
6. Hati za matokeo za kidato cha nne, sita na vyuo (Testmonials, Provisional
Results, Statement of results) HAVITAKUBALIWA.
7. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
8. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
9. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi haukubaliki watakaohusika
watachukuliwa hatua za kisheria.
10.Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 18 Novemba, 2025.
11.Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na
vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU WA BUNGE,
OFISI YA BUNGE,
10 BARABARA YA MOROGORO,
S.L.P. 941,
40490 TAMBUKARELI,
DODOMA.
12.Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia
inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
13.Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.
PAKUA HAPA PDF YA TANGAZO












