Haya Hapa Mambo gani muhimu yanapaswa kuzingatiwa wakati wa kuomba mkopo HESLB.
- Hakikisha umesaini fomu ya maombi ya mkopo
- Hakikisha mdhamini wako amesaini fomu yako katika eneo lake
- Hakikisha fomu yako imesainiwa na kugongwa mihuri na Serikali ya Mtaa au Kijiji chako
- Hakikisha fomu yako imesainiwa na mwanasheria au hakimu kuthibitisha taarifa zako na za mdhamini wako
Vidokezo vya Kuongeza Nafasi Yako ya Kupata Mkopo
- Hakikisha taarifa zote ni sahihi na zinalingana na admission yako.
- Tumia index number sahihi ya NECTA.
- Lipa ada kwa wakati ili usikose fursa.
- Fuatilia status yako kwenye OLAMS mara kwa mara.
- Ikiwa umekataliwa, unaweza kuomba appeal kwa kufuata taratibu.
Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti rasmi: https://www.heslb.go.tz/







