Home NACTVET NACTVET Online Application 2025/2026: Jinsi Kutuma Maombi ya Udahili Vyuo NACTVET

NACTVET Online Application 2025/2026: Jinsi Kutuma Maombi ya Udahili Vyuo NACTVET

423
0

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) lina jukumu kubwa katika mfumo wa elimu nchini Tanzania. NACTE/ NACTVET inachukua nafasi muhimu katika kuimarisha na kusimamia elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi ambayo yanajumuisha programu za vyeti, diploma, na shahada. Lengo kubwa la baraza hili ni kuhakikisha utoaji wa mafunzo yaliyo bora kwa kuzingatia viwango vya kitaifa na kimataifa.

Programu zinazotolewa na vyuo vya NACTE zinatofautiana katika viwango, yakiwemo mafunzo ya cheti, diploma, na shahada. Waombaji wote wa vyuo vya NACTE wanatakiwa kuhitimu kidato cha nne au cha sita na kuwa na angalau ufaulu katika masomo yasiyo ya kidini. Kwa program maalum kama vile Utabibu, waombaji wanatakiwa kuwa na sifa maalum za masomo ya sayansi kama Kemia na Baiolojia.

Ili kutuma maombi ya udahili kwa vyuo vya NACTE, waombaji wanatakiwa kukidhi vigezo fulani kulingana na programu wanayoomba. Kwa ujumla, waombaji wanapaswa kuwa na:

Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE): Waombaji wanapaswa kuwa na angalau ufaulu wa masomo manne (4) yasiyo ya kidini.

Kwa Wale Walio na Cheti cha Technician (NTA Level 4): Wanapaswa kuwa na cheti kinachotambulika katika fani husika kutoka taasisi zinazotambulika na NACTE.

Kwa Wale Walio na Advanced Certificate of Secondary Education Examination (ACSEE): Waombaji wanahitajika kuwa na angalau ufaulu katika somo moja kuu na ufaulu unaofuatia katika somo kuu jingine.

Cheti cha Ufundi/National Vocational Award (NVA) Level III: Pia, wale wenye cheti hiki wanaweza kutuma maombi kwa programu zinazojumuisha mafunzo ya ufundi.
Ratiba za Mchakato wa Udahili wa Vyuo vya NACTE kwa Mwaka  wa masomo 2025/2026

Tembelea Tovuti ya NACTE:
Kwenye kivinjari chako, andika anwani ya tovuti rasmi ya NACTE Central Admission System: CAS >> https://tvetims.nacte.go.tz/

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here