HATUA ZA KUOMBA BARUA YA UTAMBULISHO
SEHEMU YA KWANZA: Muombaji.
C. Hatua za kutuma maombi kupitia USSD
i. Mwombaji ataingia kwenye menu ya huduma za kiserikali *152*00#
ii. Atachagua namba 3 Ajira na Utambuzi
iv. Atachagua namba 7 Anwani za Makazi
v. Atachagua namba 4 Maombi ya barua ya utambulisho
vi. Atachagua namba 1 Omba anwani yako
vii. Atachagua namba 1,2 au 3 ili kuingiza NIDA, Namba ya Simu au TIN,
viii. Baada ya hapo mfumo utatuma OTP kwenye namba ya simu ya mwombaji
ix. Mwombaji atafuata tena hatua zote mpaka hatua ya 4 kisha atachagua 2 kamilisha maombi kwa OTP na kuandika OTP alotumiwa mwombaji
xii. Atachagua anwani yake na,
xiii. Kisha ataandika jina la mkoa ambapo taasisi anayopeleka barua inapatikana na ataandika jina la taasisi hiyo na kuchagua anwani ya hiyo taasisi,
xiv. Mwombaji atapokea ujumbe wenye namba ya ufuatiliaji ambapo atainakili.
SEHEMU YA PILI: MTENDAJI MTAA KUIDHINISHA
Mtendaji wa Mtaa au Kijiji anaweza kuidhinisha maombi ya barua ya utambulisho kwa kutumia wavuti na programu tumizi. Hatua ni kama ifuatavyo:
i. Mtendaji wa Mtaa au Kijiji ataingia kwenye wavuti au programu tumizi ya NaPA kwa akaunti yake yenye jukumu la mtendaji wa mtaa/Kijiji.
ii. Atachagua menyu ya maombi ya utambulisho kisha atachagua ombi husika.
iii. Kisha atapitisha ombi la barua.
SEHEMU YA TATU: MWANANCHI KUPAKUA BARUA Mwananchi anaweza kufuatilia ombi lake la barua na kufahamu hali ya utekelezaji kutumia nambari ya ufuatiliaji.
Hatua ni kama ifuatavyo:
i. Mwombaji ataingia kwenye mfumo wa NaPA kupitia wavuti au programu tumizi.
ii. Ataingiza namba ya ufuatiliaji ombi ikiwa ombi limepitishwa ataona kitufe cha kupakua barua.






