TANGAZO LA KURIPOTI SHULE YA POLISI MOSHI KWA
VIJANA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI
TANZANIA
1. Mkuu wa Jeshi la Polisi anawatangazia vijana waliochaguliwa kujiunga na
Jeshi la Polisi Tanzania kuwa wanatakiwa kuripoti Shule ya Polisi Moshi
kuanzia tarehe 12/06/2025 hadi tarehe 14/06/2025 kwa ajili ya kuhudhuria
mafunzo.
2. Vijana waliofanyiwa usaili Dar es Salaam kwenye Vikosi vilivyo chini ya
Makao Makuu ya Polisi wataripoti jijini Dar es Salaam katika uwanja
wa gwaride uliopo Kambi ya Polisi (Police Barracks) barabara ya
Kilwa nyuma ya kituo cha Polisi Kilwa Road tarehe 12/06/2025 saa
12.00 asubuhi kwa ajili ya safari ya kwenda Shule ya Polisi Moshi.
3. Vijana waliofanyiwa usaili Mikoa ya Tanzania Bara wanatakiwa kuripoti
kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa waliofanyia usaili tarehe 11/06/2025
saa 2.00 asubuhi kwa ajili ya kupewa utaratibu wa safari ya kwenda Shule
ya Polisi Moshi.
4. Vilevile, vijana waliofanyia usaili Zanzibar (Unguja na Pemba)
wanatakiwa waripoti Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani) tarehe
11/06/2025 saa 2.00 asubuhi kwa ajili ya kupangiwa utaratibu wa safari.
5. Aidha, vijana wote waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti Shule ya Polisi
Moshi wakiwa na vifaa vifuatavyo:
i) Traki suti (track suit) rangi ya bluu (blue) yenye ufito mweupe, fulana
(t-shirt) nyeupe isiyo na maandishi, raba, soksi nyeusi, bukta mbili
(2) za bluu (blue) kwa ajili ya michezo na mazoezi pamoja na
sanduku la chuma (Tranka) la rangi ya bluu.
ii) Chandarua cheupe cha duara na sio cha pembe nne, shuka za rangi ya
bluu mpauko (light blue) jozi mbili (Shuka 4), pasi ya mkaa na
blanket moja la kijivu lisilo na maua na sio duveti.
iii) Kikombe cha plastiki ambacho kimetengenezwa kwa matirio ya
mfupa (Cream light), Sahani moja aina ya ‘steel dish plate’.
iv) Vifaa vya usafi: Sururu moja lenye mpini, ndoo mbili ndogo na fagio
la chelewa.
v) Kadi ya bima ya Afya (NHIF) kama anayo au fedha taslimu Tsh.
50,400/= kwa wasio na kadi za bima ya Afya.
vi) Vyeti halisi vya taaluma (Original Academic Certificates), cheti
halisi cha kuzaliwa, kadi ya NIDA au namba ya Utambulisho wa
Taifa (NIDA), Nakala za kadi za NIDA au namba za Utambulisho wa
Taifa (NIDA) za wazazi na watu wa karibu upande wa Baba na Mama
(kama vile Baba, Baba mkubwa, Baba mdogo, Shangazi, Mama,
Mama mkubwa, Mama mdogo, Mjomba, Babu nk), passport size 6
(background blue), na nakala (copy) 5 kwa kila cheti kilichoainishwa
hapo juu.
vii) Fedha za kujikimu.
PAKUA MAJINA HAPA PDF YA MAJINA
6. Simu za mkononi haziruhusiwi chuoni, hivyo ni marufuku kuripoti Shule
ya Polisi Moshi ukiwa na simu ya mkononi. Yeyote atakayepatikana na
simu itachukuliwa kuwa ni utovu wa nidhamu na adhabu yake ni
kufukuzwa mafunzo mara moja. Shule itaelekeza utaratibu wa kupata
mawasiliano.
7. Kwa yeyote atakayeripoti Shule ya Polisi Moshi baada ya tarehe
14/06/2025 hatopokelewa na atahesabika amejiondoa mwenyewe kwenye
mafunzo.
8. Orodha ya vijana waliochaguliwa imeambatishwa kwenye tangazo hili.
Imetolewa na;
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania,
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,
S.L.P 961,
DODOMA.
01/06/2025.








