Fahamu jinsi ya kuomba chuo cha afya ngazi ya Astashahada (Certificate) na Stashahada (Diploma). Maombi ya udahili wa vyuo vya afya hufanyika kwa njia ya mtandao kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System – CAS) unaosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET).
MAELEZO MUHIMU
1. Katika kipindi cha kutuma maombi, lazima uwe na email hai inayofanya kazi; na nambari ya simu ya mkononi.
2. Tafadhali chagua Programu unayoipenda zaidi kulingana na sifa zako.
3. Unaweza kuchagua hadi taasisi/programu 12.
4. Ada ya Maombi ni Tsh.15,000/= kwa kila taasisi na kiwango cha juu cha Tsh.45,000/= kwa machaguo yaliyobaki (Hazirejeshwi).
5. Utapewa Control Namba kwa ajili ya malipo ya Ada ya Maombi.
6. Malipo yanaweza kufanywa kupitia huduma za Pesa za Simu au Benki.
7. Tafadhali soma Kitabu cha Mwongozo wa Uandikishaji wa Wanafunzi (Guide Book) kwa ajili ya sifa/vigezo maalum vya kuomba kozi yako kabla ya kufanya chaguo lolote.
Bofya hapa ili kutazama/kupakua Kitabu cha Mwongozo wa Uandikishaji (Guide Book).







