Home JESHI LA UHAMIAJI Sifa za Ujumla Kazi Jeshi la Uhamiaji December 2025

Sifa za Ujumla Kazi Jeshi la Uhamiaji December 2025

285
0
📢 JIUNGE NA CHANNEL YETU

TANGAZO LA AJIRA
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kwa Mamlaka niliyonayo chini ya Kanuni Namba
11(1) ya Kanuni za Uendeshaji za Uhamiaji za Mwaka 2018, natangaza nafasi za
Ajira Mpya za Konstebo wa Uhamiaji kwa Vijana wa Kitanzania wenye sifa
zifuatazo:-
1. SIFA ZA MWOMBAJI
i. Awe ni raia wa Tanzania;
ii. Awe hana ajira au hajawahi kuajiriwa na Taasisi yoyote Serikalini;
iii. Awe na Cheti cha Kuzaliwa;
iv. Awe na Kitambulisho cha Taifa au namba ya utambulisho iliyotolewa na
Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA);
v. Awe na siha njema ya mwili na akili.
vi. Awe hajawahi kutumia Dawa za kulevya;
vii. Asiwe na kumbukumbu au taarifa zozote za kuhusika katika masuala au
matukio ya uhalifu au jinai;
viii. Asiwe na alama yoyote au michoro (Tatoo) katika mwili wake;
ix. Awe hajaoa au kuolewa wala kuwa na mtoto;
x. Mwombaji mwenye Elimu ya Kidato cha Nne awe na sifa kuanzia Daraja
la kwanza (1) mpaka Daraja la tatu (3) na awe na umri kuanzia miaka 18
hadi miaka 22, Mwombaji mwenye Astashahada na Stashahada awe na
umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 25 na Mwombaji mwenye Elimu ya
Shahada/Stashahada ya Juu awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka
30.
xi. Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya Kijeshi ya Uhamiaji.
xii. Awe tayari kufanya kazi za Idara ya Uhamiaji mahali popote Tanzania.
xiii. Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za ufuatiliaji na uendeshwaji wa
zoezi la Ajira.

📢 JIUNGE NA CHANNEL YETU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here