Home ZANZIBAR Taarifa kwa Umma Kupanda kwa Nauli Za Usafiri Zanzibar Leo

Taarifa kwa Umma Kupanda kwa Nauli Za Usafiri Zanzibar Leo

13
0
📢 JIUNGE NA CHANNEL YETU

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Muhammed ametangaza kupanda kwa bei za nauli za usafiri kwa asilimia 16, ambapo nauli ya safari za kilomita moja hadi 12 imepanda kutoka shilingi 500 hadi shilingi 700.

Amesema kwa safari za umbali mrefu kuanzia kilomita 60 hadi 70, nauli itakuwa shilingi 3,000 tofauti na awali iliyokuwa shilingi 2,500.

Dkt. Khalid amesema Serikali imefanya mapitio na uchambuzi wa kina kabla ya kufikia uamuzi huo, huku ikiwashirikisha Wadau mbalimbali wakiwemo watoa huduma za usafirishaji na vyama vya usafiri ili kuhakikisha mabadiliko hayo yanazingatia hali halisi ya sekta hiyo.

Ametangaza kuwa mabadiliko hayo ya nauli yataanza rasmi kutumika kuanzia tarehe 1 Agosti Mwaka huu, sambamba na kuanza kwa huduma ya Mabasi ya Umeme.

Aidha, Dkt. Khalid amewataka Wasafirishaji kuzingatia sheria, nidhamu na usalama wa Abiria pamoja na kutunza Miundombinu ya Barabara.

Kwa upande mwengine, Dkt. Khalid amewashukuru watoa huduma za usafirishaji kwa mchango wao mkubwa kwa Wananchi, huku akisisitiza Madereva kuacha kuegesha Magari katika Vituo maalumu vitakavyotumika na Mabasi ya Umeme.

📢 JIUNGE NA CHANNEL YETU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here