VIGEZO NA MASHARTI YA KUFUNGUA NA KUENDESHA AKAUNTI YA CRDB
Classification: CRDB Internal
Utangulizi:
Haya ni makubaliano kati ya Mteja na CRDB Bank Public
Limited Company (ambayo katika makubaliano haya
itatambulika kama “CRDB” au “Benki”) kuweka vigezo
na masharti ya matumizi ya Huduma (Vigezo). Kwa
kusaini Vigezo hivi, na kuvitumia kufungua na kuendesha
akaunti, Mteja anathibitisha kwamba amesoma, ameelewa,
amekubalinayukotayarikufuata na kufungwa na Vigezo hivi.
Pia Vigezo hivi vitatumika kwa mujibu wa vigezo vingine
na masharti maalum pamoja na mwongozo wa ada na
gharama kwa muda husika. Kunapotokea kuhitilafiana
kati ya Vigezo hivi na vigezo vya huduma, masharti na
taarifa zinazohusu bidhaa/akaunti au huduma husika,
vigezo na masharti husika vitafuatwa.
Kila inapobidi CRDB itakua na hiari na wajibu wa kupitia
na kuboresha vigezo na masharti ya kufungua na
kuendesha akaunti kwa mujibu wa vigezo na masharti ya
huduma husika (ikijumuisha kiwango cha riba na gharama
nyinginezo) wakati wowote. Mteja atajulishwa
mabadiliko yoyote kama ilivyoelezwa chini ya Kifungu
cha 32.
Tafsiri ya Maneno
Ifuatayo ni tafsiri ya maneno muhimu yaliyotumika na
kuainishwa katika Vigezo hivi.
Katika Vigezo hivi; “Umoja” utajumuisha “Wingi” na
kinyume chake na Jinsia moja (kike au kiume)
itajumuisha jinsia nyingine
a) “Akaunti” inamaanisha akaunti iliyofunguliwa kwa
ridhaa ya Mteja kulingana na vigezo na masharti ya
Benki na Sheria ya Nchi.
b) “Wakala” inamaanisha kituo au kiunganishi cha
mawasiliano kati ya Mteja na Benki katika mtandao
wa usambazaji wa huduma za kibenki kama vile
Matawi yaCRDB, ATM, vituo vidogo vya huduma na
Tawi la CRDB linalohamishika(mobile branch).
c) “ATM” inamaanisha mashine ya kutolea, na au
kuwekafedha.
d) “Uhakiki” Mchakato wa kuthibitisha utambulisho wa
mtu. Uhakiki wa kidijitaliunahusisha mtu kuwasilisha
kitu au vitu kielektroniki au kuthibitisha
utambulisho wake kwamba yeye ni muhusika wa
utambulisho huo. Vitu hivyo vinaweza kuwa; Sehemu
ya mwili wake (Mfano; alama za vidole), kitu
anachojua (Mfano; nywila (PIN)), kitu anachomiliki
(Mfano; kitambulisho, au namba ya simu), au kitu
anachofanya (Mfano; mwandiko wake, au ishara za
mwili)
e) “Aliyeidhinishwa Kuweka Saini” inamaanisha
Mteja au mtu (watu) yoyote aliye na uhusiano na
Mteja ambaye Mteja amemwidhinisha na
kumtambulisha. Benki kwa maandishi ili kuendesha
Akaunti kulingana na Makubaliano, taratibu za Benki
na sheria zaNchi.
f) “Data za Maumbile/ Biometri” muonekano au
tabia za mwili wa mtu, kama vile alama za vidole,
mboni za macho, umbo la uso, mwendo, saini , n.k.
g) “Uhakiki wa Taarifa za Maumbile/Biometri” ni
njia ya kuthibitisha utambulisho inayohusisha taarifa
za maumbile/biometri au kusoma au kuchanganua
sehemuya mwili, kama vile kusoma alama za vidole
(inayojulikana kama Quick Touch), Utambulisho wa
Uso na Utamblisho wa Sauti.
h) “Utambulisho wa Data za Maumbile”
Utambulishaji wa data za maumbile kidijitali
unahusisha kulinganisha sampuli za data mpya za
maumbile na zilizohifadhiwa kabla ili kuzilinganisha
na kuthibitisha iwapo zinafanana.
i) “Kadi” inamaanisha aina zote za Kadi za
Kielektroniki zinazotolewa na Benki kutokana na
ombi la Mteja kwa ajili ya tumizi yanayohusiana na
huduma zinazotolewa na Benki, ambayo inaweza
kutumiwa Tanzania na nje ya Tanzania.
j) Mmiliki wa Kadi” inamaanisha mtu aliyepewa kadi
ya CRDB.
k) “Mteja” inamaanisha aliyetia saini nyuma ya hati hii,
nainajumuishamtuauwatu,shirika autaasisi.
l) “Namba ya utambulisho (ID)” ni namba ya siri
inayotengenezwa na mfumo na kutumwa kwa Mteja
na CRDB kwa matumizi wakati wowote Mteja
anapotumia huduma za kibenki kwa njia yamtandao
m) “Huduma za kibenki kwa njia ya mtandao”
hudumaza kibenki kupitia mtandao ni njia ya utoaji wa
huduma inayowaruhusu wateja wa benki kupata
taarifa za akaunti zao na kufanya miamala kwa njia ya
mtandao.
n) “Wakala Mkuu (Main Agent)” ni kituo cha biashara
kinachowezesha wateja kukamilisha usajili wa taarifa
zao (KYC) na kufanya miamala mbalimbali kama
vile, kuweka pesa, kutoa pesa, kutuma pesa, na malipo
ya huduma mbalimbali n.k.
o) “Mfanyabiashara (merchant)” Duka lolote la
rejareja linalopokea Kadi kwa ajili ya malipo ya
bidhaa na huduma.“Neno la siri la mara moja
(OTP)” ni neno la siri linalotumwa kwenda kwenye
VIGEZO NA MASHARTI YA KUFUNGUA NA KUENDESHA AKAUNTI YA CRDB
FOMU YA ACCOUNT YA MWANAFUNZI(CHUO AU WA KAWAIDA)
FOMU YA ACCOUNT YA MTOTO
FOMU YA ACCOUNT YA JUMUIYA/PAMOJA






