Home JKT VITU vya Kwenda navyo Waliochaguliwa Kujiunga na JKT kwa Mujibu wa Sheria...

VITU vya Kwenda navyo Waliochaguliwa Kujiunga na JKT kwa Mujibu wa Sheria 2025

423
0
📢 JIUNGE NA CHANNEL YETU

VITU vya Kwenda navyo Waliochaguliwa Kujiunga na JKT kwa Mujibu wa Sheria 2025,

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, anatoa wito kwa Vijana waliohitimu Elimu ya Sekondari Kidato cha Sita kwa mwaka 2025, kutoka Shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria kwa mwaka 2025.

JKT imewataka vijana wote Waliochaguliwa Kujiunga na JKT kwa Mujibu wa Sheria 2025 kuripoti kwenye makambi waliyopamgiwa kuanzia tarehe 28 May 2025 tarehe hadi 08 June 2025 wakiwa na vifaa vifuatavyo.

Bukta ya rangi ya ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.

T-shirt ya rangi ya kijani.

Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.

Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.

Soksi ndefu za rangi nyeusi.

Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.

Track suit ya rangi ya kijani au blue.

Nyaraka zote zinazohitajika katika Udahili wa Kujiunga na Elimu ya Juu, zikiwemo cheti vya Kuzaliwa, Vyeti vya Kuhitimu kidato cha Nne n.k

Nauli ya kwenda kuripoti makambini na kurudi nyumbani.

 

 

📢 JIUNGE NA CHANNEL YETU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here