Home JESHI LA UHAMIAJI Namna ya kufanya maombi na nyaraka za umuhimu kazi jeshi la Uhamiaji

Namna ya kufanya maombi na nyaraka za umuhimu kazi jeshi la Uhamiaji

264
0

NAMNA YA KUFANYA MAOMBI:
Maombi yote ya ajira yatawasilishwa kupitia tovuti ya Idara ya Uhamiaji ambayo
ni https://www.immigration.go.tz kuanzia tarehe 29 Desemba, 2025 na
mwisho wa kufanya maombi ni tarehe 11 Januari, 2026.
Wakati wa kufanya maombi, mwombaji anatakiwa kuambatisha (upload) kwenye
mfumo wa ajira nyaraka zifuatazo zilizo katika mfumo wa PDF (kila Nyaraka
moja isizidi 300Kb);
✓ Picha (passport size) ya hivi karibuni iliyo katika mfumo wa jpg/png isiyozidi
300Kb kwa ajili ya kuambatisha kwenye mfumo (upload);
✓ Barua ya maombi ya ajira iliyoandikwa kwa mkono;
✓ Barua ya utambulisho toka Serikali ya Mtaa/Kijiji au Shehia; kwa walio
Makambini JKT/JKU wawe na barua za utambulisho kutoka kwa Mkuu wa
Kambi;
✓ Cheti cha kuzaliwa;
✓ Awe na Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya NIDA kwa ajili ya kujisajili
kwenye mfumo;
✓ Awe na Index namba za vyeti vya kufaulu Kidato cha Nne na Kidato cha Sita
ambazo atajaza kwenye mfumo wa ajira;
✓ Awe na namba ya utambuzi ya cheti cha ngazi ya Astashahada, Stashahada,
na Shahada/Stashahada ya juu inayotambuliwa na TCU au NACTVET ambayo
atajaza namba hiyo kwenye mfumo wa ajira;
✓ Vyeti vya usajili wa taaluma kwa fani zinazohitaji usajili wa Bodi;
✓ Wasifu wa mwombaji (CV).
✓ Aidha, changamoto/maulizo wasilisha kupitia: ajira@immigration.go.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here