Home RITA RITA Gharama za huduma za usajili wa vyeti vizazi & vifo

RITA Gharama za huduma za usajili wa vyeti vizazi & vifo

406
0

RITA ni chombo cha serikali kilichokasimiwa jukumu la msingi la kusajilli Matukio Muhimu ya Binadamu ikiwemo vizazi na vifo. Jukumu hilo linasimamiwa na Sheria ya Usajili wa vizazi na Vifo Sura 108 ambayo imeweka ulazima wa kusajili kizazi na kifo kwa matukio yote yanayotokea Tanzania Bara. 

UMUHIMU WA USAJILI WA VIZAZI

(i)Kuwa na haki ya kijamii: Matokeo ya uandikishaji ni kupata cheti cha kuzaliwa ambacho kinamruhusu kupata haki mablimbali za kijamii kama kujiunga na taasisi za elimu na baadae ajira za serikali, jeshi na taasisi za umma pamoja na binafsi.

(ii)Kuwezesha kupata hati za kusafiria, kwani uhamiaji wataangalia taarifa zilizotolewa za wazazi, pamoja na kuhakikisha tarehe na mahali alikozaliwa muhusika.

(iii)Kuweza kuthibitisha umri wa mtoto au mtu kwa madhumuni ya utekelezaji wa sheria mbalimbali kama sheria ya ajira, sheria ya ndoa, sheria ya uchaguzi, sheria ya kanuni ya adhabu n.k.

(iv)Mtoto kupata haki ya utaifa ili kumwezesha kupata haki ambazo taifa linawajibika kutoa kwa raia wake.Kwa mfano, kwa sheria ya uraia ya Tanzania, endapo mzazi mmoja wa mtoto ni Mtanzania, basi mtoto huyo atakua ni raia wa Tanzania mpaka atakapofikisha umri wa miaka 18 ili aweze kuamua kama ataendelea kuwa raia wa Tanzania au vinginevyo.

(v)Kuwezesha nchi (serikali) kuweka makisio sahihi katika mipango ya kijamii na maendeleo kulingana na idadi ya watu (takwimu). Mipango hiyo ni kama vile afya, elimu, maji, uchumi, ajira, mipango ya makazi n.k.

(vi)Kuiwezesha serikali kujua �fertility rate ya mahali

(vii)Kuwawezesha ndugu wa marehemu kupata stahili za marehemu ikiwa ni pamoja na; kufungua shauri la mirathi, kufuatilia miamala ya benki, kiinua mgongo na Bima mbalimbali.

(viii)Kuwawezesha watoto wa marehemu kupata huduma za kijamii ; mfano mikopo ya elimu ya juu au misaada mbalimbali kutoka Serikalini na kwa jamii endapo itabainika watoto ni yatima.

BEI HUDUMA ZA USAJILI WA VIZAZI

NA HUDUMA ADA/GHARAMA
1 Ada ya Upekuzi 3,000
2 Kizazi kinachoandikishwa chini ya miaka kumi 8,000
3 Kizazi kinachoandikishwa baada ya miaka kumi 20,000
4 Kufanya masahihisho ya cheti cha kuzaliwa 13,000
5 Kupata nakala ya cheti kilichopotea 7,000
6 Uhakiki wa Cheti 6,000

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here