Home RITA RITA Mahitaji ya jumla kwa maombi ya cheti cha kuzaliwa

RITA Mahitaji ya jumla kwa maombi ya cheti cha kuzaliwa

391
0

RITA ni chombo cha serikali kilichokasimiwa jukumu la msingi la kusajilli Matukio Muhimu ya Binadamu ikiwemo vizazi na vifo. Jukumu hilo linasimamiwa na Sheria ya Usajili wa vizazi na Vifo Sura 108 ambayo imeweka ulazima wa kusajili kizazi na kifo kwa matukio yote yanayotokea Tanzania Bara. 

Mahitaji ya jumla kwa maombi ya cheti cha kuzaliwa:

Mwombaji lazima aambatishe baadhi ya hati mbili kati ya zifuatazo:

  • Kadi ya Kliniki ya Mama
  • Kadi ya Kliniki ya Mtoto
  • Tangazo la kuzaliwa
  • Cheti cha Ubatizo cha Mtoto (kwa wale walio batizwa wakiwa na umri mdogo)
  • Cheti cha Kumaliza elimu (Shule za Msingi au Sekondari – O Level)
  • Pasi ya kusafiria
  • Kadi ya mpiga kura
  • Cheti cha ubatizo

Pamoja na mojawapo ya haya:

  • Kitambulisho cha Kitaifa cha mzazi/mlezi
  • Hati ya kusafiria ya mzazi
  • Utambulisho kutoka Mtendaji wa Kata

N.B: Uhitaji wa kuweka vitambulisho vya wazazi vitatumika ikiwa wazazi wapo hai.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here