HUDUMA YA KUBADILISHA CHETI CHA ZAMANI KUWA KIPYA
Vyeti vya zamani ambavyo vilitolewa kabla ya vyeti vya kieletroniki vinabadilishwa kupitia huduma hii ili kuwawezesha wananchi kupata vyeti vipya vinavyotolewa kieletroniki.
JINSI HUDUMA INAVYOFANYIKA
1) Mwombaji anaweza kufanya maombi kupitia tovuti yetu www.rita.go.tz na kubonyeza menyu ya eRITA kisha kuchagua huduma inayohitajika.
2) Mwombaji atatengeneza akaunti kwa kujisajili, kisha barua pepe itatumwa kwa mwombaji ili kuthibitisha akaunti.
3) Mwombaji atahitajika kuthibitisha akaunti kwa kubonyeza kitufe kilichotumwa kwa barua pepe.
4) Mwombaji ataingia katika mfumo wa eRITA na kisha kubonyeza maombi ya kizazi baada ya hapo mwombaji atabonyeza kitufe cha �Old to New�. Baada ya hapo mwombaji atajaza taarifa zake kwa usahihi na kuchagua sehemu atakayo chukua cheti chake.
5) Mwombaji atatakiwa kuwa na nakala laini (soft copies) ya cheti chake cha kuzaliwa kinachotakiwa kuwa katika mfumo wa pdf kwa ajili ya kuambatanisha pamoja na viambata viwili kati ya vifuatavyo:
Kadi ya Kliniki ya Mama
Kadi ya Kliniki ya Mtoto
Tangazo la kuzaliwa
Cheti cha Ubatizo cha Mtoto (kwa wale walio batizwa wakiwa na umri mdogo)
Cheti cha Kumaliza elimu (Shule za Msingi au Sekondari – O Level)
Pasi ya kusafiria
Kitambulisho cha NIDA
Kitambulisho cha Mpiga kura
Pamoja na mojawapo ya haya:
Kitambulisho cha Kitaifa cha mzazi/mlezi
Hati ya kusafiria ya mzazi
N.B: Hii itatumika ikiwa wazazi wapo hai
6) Mfumo utatengeneza Control Number ya malipo ya shilingi 8,000/= kwa ajili ya kufanyia malipo.








