Iwapo mwanafunzi/Mwombaji wa mkopo hajaridhika na ki-wango cha mkopo alichopatiwa au hajapangiwa mkopo anatakiwa kufanya nini?
Fursa ya kukata rufaa hutolewa baada ya kukamilisha zoezi la kupanga mikopo
Ikitokea mwombaji akakosa kwenye rufaa, atapata fursa ya kuomba tena kwa mwaka unaofuata.
Maombi yote yanafanywa kwa njia ya mtandao wa Bodi ya Mikopo. Kila mwombaji anapaswa kusoma kwa makini mwongozo unaotolewa ndani ya mwaka husika wa masomo
Mwombaji atumie namba ya mtihani wa kidato cha nne kujisajili.
Ninawezaje kukata rufaa ya mkopo kutoka HESLB?
Rufaa lazima zinapitishwa kupitia Maafisa wa Mikopo katika Taasisi husika ya Elimu ya Juu ambao watakusanya rufaa zote kutoka taasisi yake husika na kuziwasilisha chini ya barua ya maombi kwa Bodi.







