Home RITA RITA Jinsi ya kubadilisha cheti cha zamani kuwa kipya

RITA Jinsi ya kubadilisha cheti cha zamani kuwa kipya

818
0

HUDUMA YA KUBADILISHA CHETI CHA ZAMANI KUWA KIPYA

Vyeti vya zamani ambavyo vilitolewa kabla ya vyeti vya kieletroniki vinabadilishwa kupitia huduma hii ili kuwawezesha wananchi kupata vyeti vipya vinavyotolewa kieletroniki.

JINSI HUDUMA INAVYOFANYIKA

1)    Mwombaji anaweza kufanya maombi kupitia tovuti yetu www.rita.go.tz na kubonyeza menyu ya eRITA kisha kuchagua huduma inayohitajika.

2)    Mwombaji atatengeneza akaunti kwa kujisajili, kisha barua pepe itatumwa kwa mwombaji ili kuthibitisha akaunti.

3)    Mwombaji atahitajika kuthibitisha akaunti kwa kubonyeza kitufe kilichotumwa kwa barua pepe.

4)   Mwombaji ataingia katika mfumo wa eRITA na kisha kubonyeza maombi ya kizazi baada ya hapo mwombaji atabonyeza kitufe cha �Old to New�. Baada ya hapo mwombaji atajaza taarifa zake kwa usahihi na kuchagua sehemu atakayo chukua cheti chake.

5)    Mwombaji atatakiwa kuwa na nakala laini (soft copies) ya cheti chake cha kuzaliwa kinachotakiwa kuwa katika mfumo wa pdf kwa ajili ya kuambatanisha pamoja na viambata viwili kati ya vifuatavyo:

Kadi ya Kliniki ya Mama

Kadi ya Kliniki ya Mtoto

Tangazo la kuzaliwa

Cheti cha Ubatizo cha Mtoto (kwa wale walio batizwa wakiwa na umri mdogo)

Cheti cha Kumaliza elimu (Shule za Msingi au Sekondari – O Level)

Pasi ya kusafiria

Kitambulisho cha NIDA

Kitambulisho cha Mpiga kura

Pamoja na mojawapo ya haya:

Kitambulisho cha Kitaifa cha mzazi/mlezi

Hati ya kusafiria ya mzazi

N.B: Hii itatumika ikiwa wazazi wapo hai

6)    Mfumo utatengeneza Control Number ya malipo ya shilingi 8,000/= kwa ajili ya kufanyia malipo.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here