Home VETA Utaratibu wa Kujiunga na Kozi za Muda Mrefu Kwenye Vyuo vya Veta

Utaratibu wa Kujiunga na Kozi za Muda Mrefu Kwenye Vyuo vya Veta

175
0

VETA imeweka utaratibu na sifa za kujiunga na kozi za muda mrefu kama ifuatavyo:

Nafasi za kujiunga na masomo hutangazwa mwezi wa Agosti kila mwaka. Matangazo hutolewa katika vyombo vya habari nchini pamoja na kwenye tovuti ya VETA yaani www.veta.go.tz

  1. Mwombaji ni lazima awe amemaliza elimu ya msingi, sekondari na kuendelea;
  2. Mwombaji huchukua fomu katika chuo chochote kilichopo karibu. Fomu hizo zina taarifa ya vyuo vyote vinavyomilikiwa na VETA, ikiwa ni pamoja na fani zinazofundishwa na mahali chuo kilipo na kama ni kutwa au bweni;
  3. Mwombaji anaruhusiwa kufanya mtihani wa kujiunga mkoa aliochukua fomu lakini anaweza kuchagua kusoma mkoa wowote anaochagua kulingana na mahitaji yake;
  4. Mwombaji anatakiwa kufanya mtihani wa kujiunga (Aptitude Test) mwezi Oktoba na wale wanaofanikiwa kuchaguliwa hupewa taarifa mwezi Desemba ili kuanza masomo mwezi Januari mwaka unaofuata;
  5. Mwombaji anayefanikiwa hupewa barua ya kujiunga inayofafanua mahitaji yote muhimu. Mahitaji yanatofautiana toka chuo kimoja hadi kingine na kutegemeana na fani aliyoomba, na pia kama ni kutwa au bweni;
  6. Kwa utaratibu huu Mwombaji anaanza kujiunga na ngazi ya 1 (Level 1) ambayo ni ngazi ya chini. Waombaji wanaoendelea na ngazi za juu (Level II – III) vigezo ni ufaulu wa ngazi husuka unamwezesha kupanda ngazi nyingine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here