MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI NGAZI YA TATU KATIKA VYUO VYA VETA KWA MUHULA WA MAFUNZO UNAOANZA TAREHE 14 JULAI 2026
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inapenda kuutaarifu umma kuwa uchaguzi wa waombaji wa kujiunga na Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi ngazi ya tatu katika vyuo vya VETA kwa muhula wa mafunzo unaoanza tarehe 14 Julai, 2026 umekamilika kwa awamu ya kwanza.
Orodha ya majina ya waliochaguliwa na fomu ya maelekezo ya kujiunga (Join Instruction) inapatikana kwenye tovuti ya VETA, www.veta.go.tz na kwenye vyuo vya VETA kote nchini.
Waombaji wote waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti katika vyuo walivyopangiwa na kukamilisha taratibu za usajili kabla ya tarehe 14 Julai, 2026 ili kuanza masomo rasmi.
Pakua pdf hapo chini







