Home RITA RITA Jinsi ya kufanya marekebisho vyeti vya kuzaliwa

RITA Jinsi ya kufanya marekebisho vyeti vya kuzaliwa

376
0

MAOMBI YA KUFANYA MAREKEBISHO KATIKA VYETI VYA KUZALIWA

Huduma hii kwa sasa haipo kieletroniki na hivyo kuhitaji mwombaji kufika katika Ofisi zetu za Makao Makuu au Wilaya.

Marekekbisho ya Jina la Mtoto

Marekebisho katika ya Sheria Usajili wa Vizazi na Vifo Sura ya 108 yaliyofanyika mwaka 2019, na kuruhusu marekebisho ya majina ya mtoto pale ambapo kizazi kilisajiliwa kabla ya kupewa jina au kizazi kilisajiliwa na kupewa jina lakini jina hilo limebadilishwa, mzazi au mlezi anaweza, muda wowote kabla mtoto hajafikisha miaka 18 kupeleka maombi kwa Msajili ya kutaka jina libadilishwe.

Maombi hayo yatawasilishwa kwa barua kwa Msajili Mkuu na kuambatisha nyaraka za uthibitisho pamoja na kulipia ada iliyowekwa, na endapo maombi yatakidhi vigezo marekebisho hayo yatafanyika katika daftrari la usajili.

Angalizo; Jina linalobadilika ni la mtoto na sio majina ya wazazi.

Marekebisho ya herufi kwenye cheti cha kuzaliwa

Marekebisho ya herufi zilizokosewa kwenye cheti yanawezekana kufanyika kwa mwombaji kuwasilisha barua na viambatisho vinavyoonesha usahihi wa taarifa zake ili aweze kufanyiwa marekebisho kama yatakidhi vigezo. Endapo jina lililokosewa ni la mzazi mwombaji awasilishe kitambulisho cha mzazi husika, kama taarifa ni za mwombaji mwenyewe atawasilisha vitambuliisho vyake mfano cheti cha ubatizo, kadi la Klinik, vyeti vya shule N.K.

MAHITAJI YA JUMLA

  • Barua ya kuomba marekebisho
  • Cheti halisi kinachotakiwa kurekebishwa

 Viambata vinavyothibitisha marekebisho yanayohitajika kama jina lililokosewa ni la mzazi utakuja na kitambulisho cha mzazi husika kama taarifa ni zako utakuja na vitambuliisho vyako mfano cheti cha ubatizo, kadi la clinic, vyeti vya shule.

  1.  Affidavit inaweza kuhitajika
  2. Ada ya malipo ya shilingi 13,000/=

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here