Home ZHESLB Taarifa Kwa Umma – Dirisha La Uombaji Mikopo 2026/2027

Taarifa Kwa Umma – Dirisha La Uombaji Mikopo 2026/2027

23
0
📢 JIUNGE NA CHANNEL YETU

TAARIFA KWA UMMA – DIRISHA LA UOMBAJI MIKOPO 2026/2027

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU ZANZIBAR (BMWEJZ / ZHESLB)

Tarehe: 03 Julai, 2026

DIRISHA LA UOMBAJI MIKOPO LIMEFUNGULIWA

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Zanzibar inawataarifu umma kuwa Dirisha la maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2026/2027 limefunguliwa rasmi.

VIWANGO VYA MASOMO YANAYOKUBALIWA

Maombi yanakubalika kwa viwango vifuatavyo:

  • Diploma
  • Digrii (Degree)
  • Masters
  • PhD

TAREHE MUHIMU

 

Aina ya Maombi Tarehe ya Kufungua Tarehe ya Kufunga
Mikopo ya Ndani ya Nchi (Tanzania) 03 Julai, 2026 31 Agosti, 2026
Mikopo ya Nje ya Nchi (Abroad) 03 Julai, 2026 31 Julai, 2026

MAELEKEZO KWA WAOMBAJI

  1. Soma Muongozo Vizuri – Waombaji wote wanaombwa kusoma vizuri muongozo wa uombaji mikopo unaopatikana kwenye tovuti rasmi ya Bodi.
  2. Tovuti Rasmi: www.zheslb.go.tz
  3. Jinsi ya Kuwasilisha Maombi: Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa ZOLAS (ZHESLB Online Loans Application System).
  4. Kiunganishi (Link) cha Kuwasilisha Maombi:

https://zolas.zheslb.go.tz/zolas

MUHIMU KUKUMBUKA

  • Hakikisha umeomba ndani ya muda uliopangwa.
  • Maombi yaliyowasilishwa baada ya tarehe ya mwisho hayatakubaliwa.
  • Fuata taratibu zote zilizoainishwa kwenye muongozo wa uombaji mikopo.
  • Hakikisha umesoma na kuelewa muongozo kabla ya kuanza mchakato wa kuomba.

 

WITO KWA WAOMBAJI

Bodi inawahimiza waombaji wote kuchukua fursa hii na kuwasilisha maombi yao mapema ili kuepuka msongamano wa dakika za mwisho.

Imetolewa na:

Kitengo cha Habari, Taaluma na Uhusiano
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Zanzibar

“LIPA MKOPO NA WENGINE WASOME”

© 2026 Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Zanzibar. Haki zote zimehifadhiwa.

 

 

 

 

 

 

 

📢 JIUNGE NA CHANNEL YETU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here