Home ZHESLB MUONGOZO WA MAOMBI YA UFADHILI NA MKOPO WA SMZ 2026/2027

MUONGOZO WA MAOMBI YA UFADHILI NA MKOPO WA SMZ 2026/2027

16
0
📢 JIUNGE NA CHANNEL YETU

1.0 UTANGULIZI

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Zanzibar (BMWEJZ) ni Taasisi ya Serikali inayojitegemea ikiwa chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali (WEMA). Imesajiliwa chini ya Sheria Namba 2 ya mwaka 2024 baada ya kufutwa Sheria Namba 3 ya mwaka 2011.

Bodi ina jukumu la kutoa mikopo pamoja na ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na kati, pamoja na kukusanya marejesho ya mikopo ili kuufanya utaratibu wa utoaji mikopo kuwa endelevu.

Waombaji mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2026/2027 wanatakiwa kusoma na kuuelewa Muongozo huu kabla ya kutuma maombi ya mkopo.

 

2.0 MAELEKEZO MUHIMU KWA WAOMBAJI WAPYA WA UFADHILI WA SMZ

Waombaji wote wa ufadhili wa SMZ kwa mwaka wa masomo 2025/2026 watapaswa kuwasilisha maombi yao kupitia mfumo maalum wa maombi ya mtandaoni unaojulikana kama ZHESLB Online Loans Application System (ZOLAS).

Mfumo wa ZOLAS umeunganishwa na mifumo ya taasisi nyingine za Elimu ya Juu, zikiwemo:

  • Tume ya Taifa ya Vyuo Vikuu (TCU)
  • Baraza la Mafunzo ya Ufundi (NACTVET)
  • Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA)
  • Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania (HESLB)
  • Mamlaka ya Usajili wa Matukio ya Kijamii ya Zanzibar (ZCSRA)
  • Mfumo wa malipo wa Serikali (ZANMALIPO)

Masharti ya Kutuma Maombi:

  1. Kuwa na Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi.
  2. Kuhakiki vyeti vyao vya kuzaliwa ZCSRA na kupatiwa Nambari maalum (Token) kwa wasiofikia umri wa miaka 18.

iii. Nambari ya mtihani wa kidato cha nne iwe sawa na nambari aliyoituma kuwasilisha maombi ya kujiunga na chuo.

  1. Majina matatu yanayotumika kwenye Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi na kidato cha nne yanalingana.
  2. Kuwa na baruapepe (email) binafsi na ambayo haitobadilika kwa wakati wote. Waombaji wanasisitizwa kuhifadhi vizuri neno siri (password) zao.

 

3.0 MAELEKEZO YA KUJAZA MAOMBI

3.1 Usajili wa Akaunti

Mwombaji atatakiwa kujisajili kwenye mfumo wa ZOLAS kwa kutumia namba yake ya Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi. Kwa mwanafunzi ambaye hakutimia miaka 18, atatumia Nambari ya cheti cha kuzaliwa kama jina la utambulisho (username).

3.2 Kutuma Maombi

Ufunguzi wa akaunti unamwezesha mwombaji kutuma maombi kwa kufuata maelekezo yaliyopo na kujaza kikamilifu kila kipengele husika ikiwa ni pamoja na kuwasilisha (submit) ombi lake.

Tanbihi: Maombi ya ufadhili ni bure. Inashauriwa waombaji kuomba mkopo pia kwani nafasi za ufadhili huwa chache na wahitaji ni wengi. Ukiwa hukuomba mkopo na ufadhili wa SMZ umekosa, utakuwa huwezi kupata fursa ya kupatiwa mkopo ambao hukuuomba.

 

3.0 SIFA ZA KUPATA UFADHILI WA SMZ

Waombaji wa ufadhili wa SMZ ambao maombi yao yanaweza kuzingatiwa wakati wa uteuzi ni:

  1. a) Awe Mzanzibari.
  2. b) Ame wasilisha maombi yake kupitia mfumo wa mtandao wa BMWEJZ ndani ya muda maalum uliowekwa.
  3. c) Awe na ufaulu mzuri zaidi wa daraja la kwanza katika mitihani ya Taifa ya kidato cha sita.
  4. d) Ame pata udahili kwenye Taasisi ya Elimu ya Juu iliyopo Tanzania.
  5. e) Amedahiliwa miongoni mwa fani za vipaumbele vya Taifa (Kiambatisho Na. 1).
  6. f) Asiwe na mkopo au udhamini wa masomo kutoka taasisi nyingine.
  7. g) Amemaliza masomo ya kidato cha sita katika mwaka husika wa ufadhili.
  8. h) Amemaliza masomo yake ya kidato cha sita kutoka Shule za Sekondari zilizopo Zanzibar.

 

4.0 UTEUZI WA WANUFAIKA WA UFADHILI WA SMZ

Uteuzi wa wanufaika wa ufadhili wa SMZ kwa mwaka 2026/2027 utaendelea kufanyika kwa kuzingatia mgawanyo wa wanafunzi waliopata ufaulu wa daraja la kwanza katika mitihani ya kidato cha sita baina ya Shule za Serikali na Shule za Binafsi zilizoko Zanzibar kwa mwaka husika.

Tanbihi: Kwa mwanafunzi ambaye atakuwa amepata Ufadhili wa SMZ pamoja na Ufadhili wa Samia (Samia Scholarships), ataondolewa katika ufadhili wa SMZ na nafasi yake kutumika kwa wanafunzi wenzake wahitaji.

 

4.1 KUTANGAZWA MAJINA YA WANUFAIKA WA SMZ

Taarifa za wanafunzi wote walioteuliwa zinatarajiwa kutoka ndani ya mwezi wa Oktoba 2026 na zitakuwa zikipatikana katika akaunti za wanafunzi husika ambazo zimetumika kuombea ufadhili wa SMZ. Aidha, taarifa hizo huwasilishwa katika vyuo husika kwa hatua zaidi.

 

5.0 KUJAZA MIKATABA

Mkataba ni hati ya makubaliano baina ya BMWEJZ na mwanafunzi ambapo BMWEJZ itampatia mnufaika wa ufadhili wa SMZ mafao stahiki baada ya muombaji huyo kutimiza masharti yote yaliyoainishwa kwenye Mkataba.

5.1 MIKATABA YA WANUFAIKA WAPYA WA SMZ

Waombaji wapya walioteuliwa kupata ufadhili wa SMZ watapaswa kujaza mikataba na kulipia ada ya Mkataba ya TZS 35,000 kupitia Benki ya PBZ au wakala wa Benki hiyo.

Mwombaji aliyeteuliwa atapaswa kuingia kwenye akaunti yake aliyoitumia wakati wa kuwasilisha maombi ya ufadhili wa SMZ. Muda wa kujaza Mikataba mipya ni baada ya uteuzi ambao utaanzia mwezi wa Oktoba hadi Desemba 31, 2026.

Kupitia akaunti hiyo, mwombaji atapatiwa nambari maalum ya kumbukumbu ya kufanya malipo (Control Number) kabla ya kuendelea na hatua nyingine za kujaza mikataba.

5.2 MIKATABA YA WANUFAIKA WANAOENDELEA NA MASOMO

Wanufaika wa ufadhili wa SMZ wanaoendelea na masomo mwaka 2026/2027 katika Taasisi mbalimbali za Elimu ya Juu, watapaswa kuhuisha taarifa zao kulingana na mwaka wa masomo uliopo pamoja na kuwasilisha matokeo ya mwaka uliomalizika. Hakutakuwa na gharama za kulipia mkataba mpya.

Muda wa kuhuisha taarifa zao utaanza Agosti 1 hadi Septemba 30, 2026.

Tanbihi: Kwa mwanafunzi ambaye hatohuisha taarifa zake kwa wakati, atakuwa amejiiondoa katika udhamini wa masomo kupitia BMWEJZ.

 

6.0 MAFAO KWA WANUFAIKA WA UFADHILI WA SMZ

6.1 Vipengele vya Mafao

 

 

Na. Mafao kwa wanufaika wa Ufadhili wa SMZ Kiwango cha Malipo TZS
1. Ada ya masomo Yote
2. Ada ya mitihani Yote
3. Posho la chakula na malazi 1.5M Zanzibar, 1.8M Tz Bara
4. Mahitaji maalum ya kitivo (Special faculty requirement) Si zaidi ya 300,000
5. Bima ya afya 50,400
6. Posho la vitabu na viandikwa (Stationery) 200,000
7. Mafunzo kwa vitendo 300,000

6.2 Utaratibu wa Malipo

Posho la chakula na malazi, Bima ya afya, Posho la vitabu na viandikwa, mahitaji maalum ya kitivo na mafunzo kwa vitendo zitalipwa moja kwa moja kwenye akaunti ya benki ya mwanafunzi husika.

Ada ya masomo na mitihani zitalipwa moja kwa moja kwenye akaunti ya benki ya Taasisi husika.

Tanbihi: Inasisitizwa mwanafunzi kuwasilisha nambari yake binafsi ya akaunti kwa usahihi ambayo ipo hai (active).

6.3 Maombi Kupitia Vituo vya Usaidizi (One Stop Center)

BMWEJZ kwa mwaka 2026/2027 imesitisha ufunguzi wa vituo vya usaidizi na badala yake itajikita katika kuwapa uelewa wanafunzi wahitaji kupitia makundi tofauti. Kwa watakaokuwa na changamoto, milango iko wazi kuwasiliana na Bodi au hata kufika kwa msaada zaidi. Lengo kuu ni kuwajenga wanafunzi juu ya matumizi ya mifumo ambayo ndiyo chachu ya maendeleo kwa sasa.

 

7.0 UTARATIBU WA WANAFUNZI WANAOREJEA MWAKA

Wanafunzi watakaorejea mwaka husika wa masomo kwa ufadhili wa SMZ watalazimika kuwasilisha barua rasmi kutoka chuoni inayothibitisha uwepo wa taarifa hizo. Uongozi wa BMWEJZ ukiridhia mwanafunzi husika atapatiwa nyongeza ya mwaka mmoja katika miaka yake ya masomo.

Tanbihi: Fursa ya kupatiwa mkopo katika mwaka wa nyongeza kwa mwanafunzi itakuwa mara moja tu katika miaka yake ya masomo.

8.0 WADHAMINI WA WANUFAIKA WA UFADHILI WA SMZ NA WAJIBU WAO

Kila muombaji wa ufadhili wa SMZ atakayeteuliwa atalazimika kuwa na wadhamini wawili.

Sifa kuu za Mdhamini:

  • Awe Mzanzibar mwenye kitambulisho cha Mzanzibar Mkaazi
  • Ameajiriwa (angalau mdhamini mmoja)
  • Awe na kitambulisho cha ZSSF au Kazi
  • Awe hajafika miaka 55

ANGALIZO: Mwombaji atakayetoa taarifa zisizo sahihi atakuwa amekwenda kinyume na taratibu za kanuni na anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na jina lake kufutwa katika waombaji walioteuliwa kupatiwa ufadhili wa SMZ.

 

9.0 UKOMO WA UDHAMINI WA UFADHILI WA SMZ

Ufadhili wa SMZ utafika kikomo pale mnufaika atakapokumbwa na mazingira yafuatayo:

  1. a) Kashindwa kuendelea na masomo (Disco)
  2. b) Kaondoka chuoni bila taarifa
  3. c) Kasimamishwa chuo kwa sababu za kinidhamu
  4. d) Kushindwa kuwasilisha matokeo ya kumaliza mwaka
  5. e) Ameomba mwenyewe kusimamisha mkopo

ANGALIZO: Kwa mwanafunzi yoyote ambaye atabadilisha fani au chuo bila ya idhini kutoka BMWEJZ, ufadhili wake utasitishwa haraka iwezekanavyo.

10.0 MAWASILIANO

Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU, ZANZIBAR.

Kwa Mawasiliano:

Anuani:
MKURUGENZI MTENDAJI,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU,
P.O.BOX 3344,
ZANZIBAR.

 

11.0 KIAMBATISHO NA. 1: FANI ZA KIPAUMBELE

Uteuzi wa waombaji, mbali na kuangalia sifa za kitaaluma na vigezo vingine, hufanywa kwa kuzingatia vipaumbele vya Taifa ambavyo hupitiwa upya kila baada ya miaka mitatu. Fani za Vipaumbele vya Taifa kwa mwaka wa masomo 2025/26 zinajumuisha:

SEHEMU YA UALIMU (ELIMU)

  • Science and Mathematics
  • Curriculum Development
  • Fashion Design with Education
  • Technical and Vocational Teachers
  • Home Economy Teachers
  • Early Childhood and Primary Education
  • School Science Laboratory Management
  • Special Needs and Inclusive Education
  • IT with Education
  • Physical Education and Sport Professional
  • Business with Education
  • Arts and Creativity Specialists
  • Agriculture with Education
  • Geography, English, History, Kiswahili, Islamic and Divinity
  • International Languages with Education

 

SEHEMU YA AFYA (AFYA)

  • Physiotherapy
  • Global Health
  • Health Promotion
  • Biomedical Engineering
  • Entomology
  • Science in One Health
  • Dialysis Nursing
  • Public Health
  • Women’s Health Human Rights
  • Pharmacology
  • Onco-Pharmacy
  • Water Sanitation
  • Health Economic
  • Tropical Disease
  • Monitoring and Evaluation in Health
  • International Health
  • Health Management System
  • Biostatistics
  • Digital Health
  • Dental Surgery
  • Hospital Management
  • Epidemiology
  • Health Informatics
  • Ophthalmology
  • Nursing
  • Speech Therapy
  • Cardiac Nurses
  • Clinical Psychologist
  • Nutrition and Dietician
  • Environmental Health Sciences
  • Theatre Nurse
  • Food Science in Human
  • Radiology
  • Nutrition
  • Ultrasound
  • Occupational Health
  • Clinical Medicine
  • Public Health Groundwater Engineering
  • Echocardiographic and Invasive Cardiology
  • Emergency and Critical Care Nursing
  • Parasitology & Entomology
  • Biology and Technology
  • Infection Control and Tropical Diseases
  • Microbiology
  • Doctor Medicine
  • Biochemistry
  • Acupuncturist
  • Biology and Technology
  • Clinical Chemistry
  • Biotechnology
  • Diagnostic Ultrasound
  • Science Chemical Processing
  • Midwifery
  • Medicine (MD)
  • Nursing Anaesthesia
  • Bachelor of Doctor of Pharmacy
  • Prosthetics and Orthoptist
  • Medical Laboratory Technologist

 

SEHEMU YA ARDHI (ARDHI)

  • Cartography
  • Building/Construction Economics
  • Housing and Infrastructure Planning
  • Geo-informatics
  • Property and Facilities Management
  • Interior Design
  • Land Management and Valuation
  • Urban and Rural Planning Development Management
  • Land Surveying Engineering
  • Landscape Architecture
  • Land Dispute Management
  • Civil Engineering
  • Quantity Surveying
  • Architecture
  • Geotechnical Engineering
  • Geology
  • Petroleum Economics and Finance
  • Operational and Supply Chain in Oil and Gas
  • Petroleum Chemistry
  • Radiation Protection
  • Petroleum Engineering
  • Renewable Energy and Atomic Energy
  • Petroleum Law
  • Petroleum Data Management
  • Geophysics/Geochemistry
  • Hydrology
  • Petroleum Economics
  • Accounting in Oil and Gas
  • Oil and Gas Engineering
  • Drilling Engineering

 

SEHEMU YA MAJI NA NISHATI (MAJI NA NISHATI)

  • Water Engineering
  • Petroleum Reservoir Engineering
  • Water Resource Management
  • Oil and Gas Management
  • Mining Engineering
  • Offshore Engineering
  • Electrical Energy and System
  • Groundwater Engineering
  • Mechatronic Engineering
  • Hydrogeological Engineering
  • Water Supply and Sanitation Engineering
  • Water Quality Engineering
  • Solar Power Engineering
  • Water Chemistry
  • Electrical and Electronic Engineering
  • Hydrology Engineering
  • Electronic Science and Technology
  • Mineral Processing Engineering

SEHEMU YA BIASHARA NA VIWANDA (BIASHARA NA VIWANDA)

  • Trade Negotiation
  • International Economy and Trade/Finance/Commerce
  • Trade Economy and Administration
  • Metrology and Standardization
  • Corporate Finance
  • Industrial Engineering
  • Metallurgy Processing Engineering
  • Chemical Engineering
  • Architecture
  • Legal and Industrial Metrology
  • Quality Management
  • Automotive Engineering
  • Mechanical Engineering
  • Material Engineering
  • Biological/Chemical/Soil Laboratories Technicians

 

SEHEMU YA UTALII (UTALII)

  • Digital Marketing and Branding
  • Language Professions
  • Hotel Management
  • Tourism Product Development and Grading
  • Hospitality
  • International Privacy and Security in Tourism
  • Cultural Heritage Management and Conservation
  • Tourism Planning and Management
  • Antiquate
  • Architectural Conservation and Historical
  • Tourist Wildlife Management
  • Museology and Anthropology Museum Study
  • Archaeology

 

SEHEMU YA KILIMO, UFUGAJI, UVUVI NA UCHUMI WA BULUU (KILIMO, UFUGAJI, UVUVI NA UCHUMI WA BULUU)

  • Aquaculture Science/Aquatic Science
  • Forestry Economics and Management
  • Agriculture Planning
  • Agriculture Economics
  • Animal Breeding
  • Horticulture
  • Irrigation Engineering
  • Animal Nutrition
  • Agronomy
  • Marine Ecology
  • Biotechnology
  • Animal Husbandry
  • Marine Microbiology and Parasitology
  • Entomology
  • Plant Pathology
  • Coastal Engineering
  • Plant Breeding
  • Soil Science Disciplines
  • Marine Science
  • Nutrition and Food Science Technology
  • Molecular Science
  • Post-harvest Technology and Aquatic Product Processing
  • Biochemical Engineering
  • Seed Technology
  • Marine Affairs
  • Fisheries Economics
  • Microbiology
  • Marine Engineering
  • Environmental Science and Fisheries
  • Ocean Engineering
  • Technicians for Sea Machines
  • Oceanography
  • Veterinary
  • Biodiversity Conservation
  • Environmental and Coastal Management
  • Fisheries Science

 

SEHEMU YA FEDHA (FEDHA)

  • Tax Policy Analysis and Revenue Forecasting
  • Project Financial Analysis and Management
  • Tax Management
  • Digital Auditing
  • Taxation
  • Islamic Finance
  • Risk and Damage Evaluation
  • Taxation on Digital Economy
  • Islamic Insurances
  • Procurement and Supply Management
  • Financial Analyst
  • Accounting and Finance
  • Real Estate Finance and Investments
  • IT with Accounting/Business
  • Actuarial Science

SEHEMU YA HABARI, USAFIRI NA MAWASILIANO (HABARI, USAFIRI NA MAWASILIANO)

  • Maritime Transport and Nautical Science
  • Marine and Port Administration
  • Mass Communication
  • Logistics and Transport Management
  • Road Economists
  • Journalism
  • Highway Engineering
  • Maritime Business and Management
  • Sound Engineer
  • News Editor
  • Marine Navigation
  • Pilot and Aircraft Maintenance Engineering
  • Thermal Engineer
  • Mechanical Engineering
  • Nautical Architecture
  • Road Engineering and Construction
  • Maritime Law
  • Audio Visual
  • Shipping and Port Engineering
  • Marine Engineering
  • Transportation Engineering

 

SEHEMU YA TEHAMA (TEHAMA)

  • Computer and Software Engineering
  • Computer Science
  • Graphic Designer
  • System Developer
  • System Audit
  • Information Technology and Telecommunication Law
  • Robotics
  • Biometric Engineering
  • Augmented and Virtual Reality
  • Signal and Information Processing
  • Autonomous Vehicles
  • Statistical Machine Learning
  • Artificial Intelligence
  • Data Sciences
  • Database Management and Security
  • GIS
  • Network and Cyber Security
  • Computer Forensic
  • Information Communication Technology and Information Systems
  • Electronics and Telecommunication Engineering

 

LIPA MKOPO NA WENGINE WASOME

 

Mwisho wa Muongozo

 

📢 JIUNGE NA CHANNEL YETU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here